Jumanne , 25th Oct , 2016

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu ‘Rambo’ amehitimisha miaka yake mitano ya kuitumikia klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Thomas Ulimwengu

 

Ulimwengu amemaliza mkataba wake wa miaka mitano wiki iliyopita, na tayari yupo Dar es Salaam kwa mipango ya kuhamia klabu mpya, ambayo bila shaka itakuwa katika bara la Ulaya, kama mwenyewe anavyopenda

Ulimwengu, amesema anashukuru sana Mazembe, kwa miaka mitano iliyomkuza kisoka na kumfanya kwa ujumla afurahie maisha ya soka na kuwa na ndoto na tamaa zaidi.