Jumanne , 18th Aug , 2020

Timu ya Inter Milan ya Italia imefuzu kucheza fainali ya kombe la shirikisho balani ulaya jana usiku baada ya ushindi mnono wa goli tano kwa sifuri dhidi ya Shaktar Donetsk ya Ukraine.

Kocha wa Inter Milan , Antonio Conte (Pichani) akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.

Inter imefuzu kucheza fainali hizo kwa kuwafunga Shaktar Donetsk ya Ukraine kwa magoli yaliyofungwa na D'Ambrosio aliyefunga goli moja, Romero Lukaku na Lautaro Martinez wote wakifunga goli mbili kila mmoja.

Hii ni fainali ya kwanza kwa timu ya Inter Milan baada ya miaka kumi kupita, fainali ya mwisho Inter Milan ilicheza mwaka 2010 timu ilikua ikifundishwa na Jose Mourinho.

Katika Fainali ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ,Inter Milan ilipata ushindi wa goli mbili kwa sifuri ilipoifunga Bayern Munich ya Ujerumani.

Katika fainali ya mwaka huu Inter Milan itacheza na timu ya Sevilla kutokea Hispania, Mchezo wa fainali utachezwa tarehe ishirini na moja mwezi wa nane mwaka huu.

Itakua Fainali ya kwanza ya kocha wa Inter Milan Antonio Conte katika Fainali za mashindano ya Ulaya kwa ngazi ya klabu.

Inter Milan inaingia katika mchezo huo wa fainali wakijivunia safu yao bora ya ushambuliaji inayoundwa na Romero Lukaku na Lautaro Martinez.

Lukaku ambaye amekua na kiwango bora sana na timu hiyo ya Inter Milan aliyohamia kutokea Manchester United, raia huyo wa Ubelgiji ameweka rekodi mpya ya kufunga katika michezo kumi mfululizo ya kombe la Shirikisho Barani Ulaya kwa msimu huu.

Timu ya Inter Milan imefanya usajili mkubwa sana msimu huu na wamilik wa Timu hiyo wanahitaji kuona wakimaliza na taji lolote msimu huu.

Kocha Antonio Conte atahitaji kushinda kombe hili la Shirikisho kama atataka kufufua matumaini ya kubaki kuendelea kukiongoza kikosi hicho cha inter Milan kwa msimu ujao.

Conte ambaye aliwahi kuzifundisha Juventus, Chelsea na Timu ya Taifa ya Italia, alimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Serie A msimu uliomalizika, tena kwa tofauti ya alama moja dhidi ya Mabingwa , Juventus.

Baada ya msimu kumalizika, Conte alinukuliwa akimtupia mmoja ya viongozi wakuu wa klabu hiyo, akidai kuwa huenda kazi yake na hata ya wachezaji ikawa haitambuliki ,lakini pia aliamini kuwa hawakupata mtu mwenye ushawishi kwenye bodi ya ligi ambaye angesaidia kuipa nafuu ratiba yao.

Kauli hiyo ilitafsiriwa tofauti na vyanzo vingo vya habari nchini Italia viliripoti kuwa huenda Conte akafutwa kazi muda wowote baada ya kutokea sintofahamu baina yake na viongozi.

Fainali itapigwa  tarehe ishirini na moja na iwapo Inter Milan itabeba kombe mbele ya timu yenye rekodi bora katika mashindano ya kombe la shirikisho balani ulaya timu ya Sevilla,huenda mabosi wa Inter wakabadili mawazo yao dhidi ya Conte ambayo ni kumfuta kazi.

Inter itakutana na Sevilla ambayo inajivunia rekodi yake ya kushinda ubingwa wa kombe la Europa mara kwa mara.

KWA NINI TUNASEMA CONTE KATUMA UJUMBE?

-Kuiikisha Inter Fainali ya kwanza baada ya miaka 10 michuano ya ulaya

-Kumaliza nafasi ya pili katika Sere A kwa mara ya kwanza baada ya miaka 9, tena ikizidiwa alama moja pekee dhidi ya Mabingwa Juventus.

TAFSIRI YAKE

-Mabosi wa Inter wanapaswa kutafakari maneno yake hata kama yaliwakera, huenda yalikua na msingi ambao iwapo wangeyafanyia kazi, wangetwaa ubingwa wa ligi na sasa anaelekea kwenye ubingwa wa Ulaya.