
Murray baada ya kufanyiwa oparesheni, picha ya kulia ni ya X-Ray ikionesha alivyounganishiwa chuma kwenye nyonga ya kushoto.
Murray mwenye miaka 31 na bingwa wa Grand Slam mara tatu, mapema mwezi huu alitangaza kuwa huenda akaamua kustaafu baada ya michuano ya wazi ya Austaralia au michuano ijayo ya Wimbledon.
Mchezaji huyo namba moja wa zamani wa Uingereza aliweka wazi kuwa kutokana na matatizo ya nyonga yake, mchezo wake wa mwisho kwenye tenisi unaweza kuwa ule wa raundi ya kwanza aliopoteza dhidi ya Roberto Bautista Agut na kutolewa mashindanoni.
Leo ametoa ujumbe kupitia mtandano wa Instagram akielezea namna anavyopata taabu kutibu tatizo la nyonga yake lakini anaamini upasuaji aliofanyiwa unaweza kuwa tiba ya kudumu ya tatizo hilo.
''Sasa nina nyonga ya chuma, nimepata maumivu sana lakini nimepambana nayo na sasa naonekana kawaida na naamini huu ndio mwisho wa maumivu ya nyonga ambayo yamekuwa yakinisumbua sana'', amesema.
Madaktari wameeleza kuwa asilimia '90 hadi 95' ya wagonjwa ambao wanafanyiwa upasuaji wa aina hii, wanaondokana na maumivu tena maisha yao yote lakini mpaka sasa hakuna mgonjwa ambaye ametibiwa tatizo hilo na akacheza tena kwa ushindani.