Jumapili , 20th Nov , 2022

Fainali za 22 za Kombe la Dunia zimeanza rasmi nchini Qatar leo Novemba 20, 2022, ambapo katika mchezo wa ufunguzi wenyeji Qatar wamekubali kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa Ecuador.

Mshindi wa Kombe la Dunia 1998 akiwa na Ufaransa Marcel Desailly, ndiye alikabidhiwa jukumu la kuonyesha kombe la dunia halisi kwenye uwanja wa Al Bayt Qatar ambapo fainali za 22.

Magoli ya Ecuador yote yamefungwa na mshambuliaji Enner Valencia na kumfanya aingie kwenye vitabu vya rekodi kwa kufunga magoli matano ya mwisho ya Ecuador kwenye fainali za Kombe la Dunia.

Valencia anaungana na nyota wengine wa zamani akiwemo Eusebio (Ureno 1966), Paolo Rossi (Italia 1982) na Oleg Salenko (Urusi 1994) waliofunga magoli 6 mfululizo.

Mapema kwenye ufunguzi, mwimbaji staa wa Korea ya Kusini Jung Kook wa bendi ya BTS alitumbuiza kwenye ufunguzi wa fainali za kombe la Dunia 2022 katika uwanja wa Al Bayt.

Mbali na burudani ya Jung Kook, matukio mbalimbali yamefanyika kwenye ufunguzi wa fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar ikiwemo muigizaji nguli kutoka Marekani Morgan Freeman kuonekana pamoja na Mascot rasmi wa #WorldCup2022 aitwaye La'eeb.