Jumatatu , 24th Aug , 2015

Chama cha Kuogelea Tanzania TSA kimesema uchaguzi wa chama hicho uliokwamishwa na mashindano mbalimbali ndani ya chama hicho unatarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Katibu Mkuu wa TSA Noel Kihunsi amesema uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Julai mwaka huu lakini kulikuwa na maandalizi ya mashindano ya dunia yanayotarajiwa kufanyika nchini Khazan nchini Urusi huku kukiwa na mashindano ya vijana yanayoendelea hivi sasa nchini Singapore pamoja na maandalizi ya All African Games.

Kihunsi amesema, wameshakaa na kukubaliana mwezi wa uchaguzi na wameshaandaa taarifa kwa ajili ya Baraza la Michezo nchini BMT ili kuweza kufanya uchaguzi kama walivyopanga.