Jumatano , 24th Nov , 2021

Bondia anayeshikilia mkanda wa Ubingwa wa uzito wa juu ‘WBC’, Tyson Futy amefunguka kuwa, yupo tayari kurejea ulingoni mwezi Februari au Machi 2022 kutetea ubingwa huo na bondia yeyote atakayepangwa naye.

(Tyson Fury akiwa na mkanda wa ubingwa wa uzito wa juu WBC)

Fury ameibuka kuwa nambari 1 wa uzito wa juu duniani baada ya kumbonda mara mbili Deontay Wilder, lakini WBC bado haijamtangaza Dillian Whyte kama mpinzani wake wa lazima, na hivyo kumuacha bila mpinzani aliyethibitishwa.

Bondia huyo ameweka wazi kuwa yupo tayari kupambana na Whyte au mtu yoyote ambaye atakuwa na vigezo vya kupigana nae huku ndoto za kuzichapa na Joshua zikiyayuka.

Pambano ambalo limekuwa likisubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa Masumbwi kati ya Fury na Anthony Joshua, kwa sasa haliwezi kuchezwa kwasababu Joshua anatazamiwa kurudiana na Oleksander Usyk.

Joshua amekiweka hai kipengele cha mchezo wa marudiano kujaribu kurudisha mataji ya IBF, WBA na WBO ambayo alishindwa kutetea alipopiga na Oleksandr Usyk baada ya kupoteza mwezi Septemba 2021.