Alhamisi , 27th Jun , 2024

Wachezaji 20 wa kikosi cha timu ya taifa ya wanawake(Twiga Stars) wataingia kambini Julai 1, 2024 kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Tunisia na Botswana.

Wachezaji hao watakaokuwa chini ya Kocha Mkuu Bakari Shime ni Najat Abasi, Asha Mrisho, Lidya Maximilian, Protasia Mbunda, Enekia Kasonga, Juletha Singano, Vailet Mwamakamba na Anastazia Katunzi.
-
Wengine ni Joyce Lema, Janeth Christopher, Ester Maseke, Diana Lucas, Aisha Juma, Stumai Athuman, Winifrida Gerald, Maimuna Kaimu, Elizabert Charles, Aisha Masaka, Oppa Clement na Clara Luvanga.