Nahodha msaidizi, Haruna Niyonzima
Niyonzima amebainisha hayo pindi alipokuwa anazungumza na kupitia ukurasa wao wa kijamii na kudai yeye haamini historia katika ila yeye achokitazama sasa ni kuhusu mechi yao ya kesho itakayochezwa katika viunga vya Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
"Tumepoteza mchezo muhimu wa Nusu Fainali (ASFC) dhidi ya Mbao FC hivyo ushindi wa kesho dhidi ya Prisons ni muhimu sana kwanza kurudisha hamasa kwa wanachama na washabiki wetu pia kujiweka vyema kutetea ubingwa wetu, kama wachezaji tunahamasishana kwa nguvu zote ili kesho tuwe makini na kushinda mchezo huo...Kama nahodha msaidizi niwatoe hofu wadau wetu kuhusu michezo yote mitano iliyobaki tutapambana sana kushinda ili kuchukua kombe kwa mara ya tatu mfululizo. Mashabiki wajitokeze kwa wingi kesho kutupa hamasa".Niyonzima
Aidha, Niyonzima amesema mchezo wa kesho kwa upande wao wanauchukulia kama ndiyo Fainali yao baada ya kupoteza michezo mingine huku akiwataka mashabiki zao wasivunjike moyo katika kuwasapoti.
Kwa upande mwingine, Timu ya Yanga mpaka sasa imebakiwa na mechi nne mkoni ukiitoa Tanzania Prisons, kwani baada ya mechi ya kesho Yanga watazialika kwenye uwanja wa Taifa Kagera Sugar, Mbeya City, Toto Africans huku wakimaliza msimu huu ugenini kwa kuwafuata wababe wao waliowatoa katika Nusu Fainali za FA Mbao FC.

