Alhamisi , 9th Jun , 2016

Kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga Juma Mwambusi amesema, wanaendelea kuwapa mazoezi wachezaji wapya waliosajiliwa na Klabu hiyo ili waweze kuendana na utamaduni wa Yanga.

Beki wa kulia wa Yanga, Hassan Kessy

Mwambusi amesema, wamewachukua wachezaji hao sio kwa kuwatumia leo au kesho bali ni kwamuda mrefu kwani bado umri wao unaruhusu na pia wanavipaji.

Mwambusi amesema, wachezaji hao pia wanatakiwa kupata uzoefu na wachezaji waliowakuta ili kuweza kupata namba katika kikosi.

Mwambusi amesema, kwa sasa wanaendelea na harakati za kuweza kuwasajili katika shirikisho la Soka barani Afrika CAF.

Mpaka sasa Yanga imefanikiwa kuwasajili wachezaji wanne ambaye ni Hassan Kessy kutoka Simba, Vicent Andrew"Dante" kutoka Mtibwa Sugar, Juma Mahadhi kutoka Coastal Union na mlinda mlango Beno Kakolanya kutoka Tanzania Prisons ambaye bado hajaungana na kikosi kwa ajili ya mazoezi.