
Koha wa timu ya Kagera Sugar, Mecky Mexime
Mexime amebainisha hayo baada ya wadau wengi wa soka kudai timu ya Kagera itakuwa katika wakati mgumu wa kupambana na Wanajangwani kwa sababu mechi yao ya kwanza walipigwa bao 6 kwa bila.
"Matokeo ya mechi ya kwanza na Yanga ndiyo yametupa changamoto ambayo tumejiandaa vizuri nasi katika mchezo wa leo ili tuweze kupata matokeo mazuri". Alisema Mexime muda mchache walipowasili katika jiji la Dar es salaam
Aidha, Kocha huyo amesema mpaka sasa katika kikosi chake hakuna majeruhi wa aina yoyote hivyo amedai watapambana mpaka wanahakikisha wanaorudi kwao Kagera na ushindi mnono dhidi ya Yanga.