
Mwenyekiti wa CHANETA Anna Kibira amesema, wapo katika hatua ya mwisho katika kuandaa timu ambapo baada ya kumaliza michuano ya Kombe la mapinduzi visiwani Zanzibar watakuwa wamemaliza maandalizi kwa ajili ya kukamilisha ratiba.
Klibira amesema, mashindano ya Afrika yanatoa Timu tatu kutoka Afrika ambazo zitaweza kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia la vijana chini ya miaka 20 yatakayofanyika nchini Botswana.