Ijumaa , 10th Feb , 2017

Timu ya Prisons "Wajelajela" ya jijini Mbeya imesema iko tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Simba, itakayopigwa kesho JUmamosi katika dimba la Taifa dar es Salaam

Wachezaji wa Prisons wakishangilia ushindi walioupata dhidi ya Simba katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, ambapo Prisons ilishinda 2-1

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdallah Mohammed amesema wamejiandaa vilivyo kuhakikisha wanafanya vizuri na kuendeleza ubabe kwa Simba kwa kunyakua pointi tatu katika mchezo huo.

“Tunajua Simba ni timu ngumu sana lakini tumejiandaa vizuri na tunataka ushindi hata kama kuna ugumu, tutapambana kuhakikisha tunafanya vizuri,” amesema Mohammed.

Katika mzunguko wa kwanza, Simba walilala kwa mabao 2-1 mjini Mbeya na Prisons ikawa timu ya pili kuifunga Simba msimu huu baada ya African Lyon.