Ijumaa , 5th Feb , 2016

Kamati ya utendaji ya Chama cha Kuogelea nchini TSA kinatarajia kukutana hapo kesho visiwani Zanzibar katika kikao chake cha dharura kwa ajili ya kujadili juu ya katiba ya chama hicho.

Katibu Mkuu wa TSA Ramadhan Namkoveka amesema, waliteua kamati ya katiba ambayo ilitakiwa kuwasilisha katiba hiyo kwa kamati ya utendaji Januari 6 ili iweze kupigiwa kura lakini mpaka hivi sasa haijawasilishwa hivyo katika kikao hicho kitajadili ni jinsi gani ya kufanya ili katiba iweze kupitishwa.

Namkoveka amesema, katika kikao hicho watajadili pia maandalizi ya mashindano ya kufuzu michuano ya Olimpiki inayotarajiwa kufanyika mwaka huu nchini Brazili pamoja na changamoto zilizopo ikiwa maandalizi ya jumla kwa wachezaji.

Namkoveka amesema, Chama cha kuogelea cah Dunia FINA kimeandaa kozi ya makoch itakayofanyika jijini Dar es salaam hivyo katika kikao hicho watajadili ikiwa ni pamoja na kujua ni jinsi gani wataweza kupata washiriki wote kwa maana ya makocha wote ikiwa ni pamoja na kuwa na kambi ya mazoezi kwa waogeleaji wenye umri miaka 11 ili kuhakikisha wachezaji wanaoshiriki mashindano ya kimataifa kupata mafunzo yaliyo bora.

Namkoveka amesema, wataongelea pia juu ya maandalizi ya mashindano ya taifa yatakayofanyika jijini Dar es salaam ambapo mpaka hivi sasa wameshaanza maandalizi kwa kuhamasisha vilabu na wachezaji walio nje ya nchi kushiriki mashindano hayo.