Pochani kushoto Bondia Mtanzania Thomas Mashali bondia wa ngumi za kulipwa akiwajibika katika moja ya mapambano yake.
Rais wa TPBO Yasin Abdalah 'ustaadh' amesema mabondia wa ngumi za kulipwa wamekua wakipokea lawama pindi wanapopoteza mapambano yao wanayocheza nje ya nchi jambo ambalo si sahihi kwani mabondia hao wanakwenda kupigana wao binafsi na hawawakilishi nchi kama ilivyo kwa ngumi za ridhaa
Aidha Ustaadhi amesema amekua akisikitishwa sana na lawama anazosikia kupitia vyombo mbalimbali vya habari kwa wadau na baadhi ya wananchi hasa viongozi wa taasisi mbalimbali wakitupa lawama kwa mabondia mbalimbali wa ngumi za kulipwa ambao wamekua wakijigharimia wenyewe au kutegemea pesa za waratibu wa mapambano wanayoshiriki kwenda kupambana nje ya nchi na kwa bahati mbaya wanakua wakipoteza mapambano hayo
Ustaadhi amesema hakuna mtu anayetakiwa kumlaumu bondia kwa matokeo ya kupoteza pambano lake kwakua mabondia hao hawajapata msaada wowote kutoka kwa mtu yeyote hapa nchini hivyo kupiga kelele ama kumshutumu bondia kwa matokeo hayo ni kumwonea
Ustaadhi ameongeza amesema hata mabondia wanapokwenda nje ya nchi huwa wanajiwakilisha wao kwa maslai yao japo wanapotambulishwa wanatajwa nchi waliyotokea na hiyo haimaanishi kuwa anawakilisha nchi kwani matokeo ya mpambano huo katika ngumi za kulipwa ni faida na hasara kwa bondia husika na wala taifa halitahusika kwa namna yeyote katika pambano hilo na ndio maana hata wanapoondoka mabondia hao huwa hawakabidhiwi bendera ya taifa kama ilivyo kwa mabondia wa ngumi za kulipwa
Akimalizia Ustaadhi amesema ni wakati sasa kwa wadhamini, wadau na makampuni kujitokeza kudhamini ngumi za kulipwa katika suala la kuwaandaa kama ilivyokua zamani wakati wa kina Joseph Malwa, Rashid Matumla [snake Man] wakati huo akidhaminiwa katika maandalizi yake na Malinzi na hivyo kumfanya awike katika medani ya kimataifa na hapo inaweza kuwa fulsa ya mdau au hata mtu aliyemsaidia bondia kuweza kutoa lawama zake kwakua alimwezesha bondia husika na ameshindwa kufanya vema katika pambano lake.