
Torres baada ya kupata majeraha
Torres aliyeingia uwanjani akitokea benchi, aligongwa kichwa na mchezaji wa Deportivo Alex Bergantinos zikiwa zimebaki dakika tano mchezo kumalizika, na kusababisha kupoteza fahamu na kulazimu apatiwe huduma ya kwanza kwa dakika kadhaa, kisha kukimbizwa hospitali.
Kulikuwa na hofu kubwa juu ya uhai wa Torres kutoka kwa wachezaji wote wa timu mbili, huku wengine wakiogopa hata kukaribia eneo la tukio.
Lakini taarifa iliyotolewa na Atletico, mapema hii leo, imesema kuwa mchezaji huyo, hakuumia sana ndani ya kichwa, baada ya kufanyiwa vipimo vya CT Scan.