Tisa wajitokeza kuwania nafasi za uongozi TFF

Alhamisi , 10th Jun , 2021

Jumla ya watu watano wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Urais, katika Uchaguzi wa kuchagua viongozi wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF utakao fanyika Agosti 7, 2021 mkoani Tanga. Wengine wanne wamechukua fomu za kuwania nafasi za ujumbe wa kamati ya Utendaji.

Walio chukua fomu kuwania nafasi ya Urais ni Rais aliyopo madarakani anayetetea nafasi yake Wallace Karia, Evans G Mgeusa, Zahor Muhammad Haji, Oscar Oscar na Deogratus Mutungi.

Kwa upande wa wale waliochukua fomu kuwania nafasi ya ujumbe wa kamati ya Utendani ya TFF ni Lameck Nyambaya Liston Katabazi na Michael Petro hawa wote kutoka kanada namba moja (1) ya Dar es salaam, Lindi, Morogoro, Mtwara na Pwani , na kutoka kanda namba mbili (2) inayoundwa na mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga aliyechukua fomu ni Khalid Abdallah Mohamed pekee.

Jumla ya nafasi zinazowaniwa katika uchaguzi huu ni nafasi sabau nafasi moja ya Rais na nafasi sita za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF. Zoezi la kuchukua fomu bado linaendelea mpaka Juni 12, Saa 10 jioni ndio itakuwa mwisho.