Alhamisi , 7th Jan , 2016

Shirikisho la Soka Tanzania TFF limesema waandaaji wa mashindano ya kombe la Mapinduzi ambao ni Shirikisho la Soka Zanzibar ZFA wamesaidia kuzidi kukuza viwango vya soka kwa wachezaji.

Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi amesema, ZFA imesaidia kukuza soka kwa vilabu shiriki kutokana na kualika nchi tofauti ambao ni URA ya Uganda ambayo imeleta ushindani wa hali ya juu katika mashindano hayo.

Madadi amesema, juhudi hizo zimesaidia kuzifanya timu kupata ushindani ambapo pia URA inatoa sura ya kiwango cha nje ya Tanzania ambapo imesaidia timu kuweza kujijenga.

Madadi amesema, timu za Tanzania zitakazoshiriki mashindano ya CAF zimepata nafasi nzuri ya kuangalia viwango, mfumo na uwezo kwa ujumla wa timu ambapo itasaidia baada ya mashindano walimu wa timu zote husika hata ambao hawashiriki mashindano ya CAF kufanya marekebisho ya kutosha kulingana na matatizo waliyoyaona katika timu zao.