Jumatano , 11th Feb , 2015

Timu kutoka nchi sita shiriki za michuano ya Mpira wa wavu wa Ufukweni zinatarajia kuwasili nchini Februari 15 mwaka huu kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Februari 16 mpaka 18 mwaka huu.

Akizungumza na East Africa Radio, Mkurugenzi wa Kamisheni ya mchezo wa wavu wa ufukweni, Muharami Mchume amesema michuano hiyo ambayo ni sehemu ya kufuzu kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika Rio de Janeiro, Brazil mwaka 2016 itashirikisha nchi za Kenya, Burundi, Somalia, Ethiopia, Djibouti na wenyeji Tanzania.

Mchume amesema, timu shiriki ya hapa nchini imeshaingia kambini na inaendelea na mazoezi na wanaamini kutokana na mazoezi hayo wataweza kufanya vizuri katika mihuano hiyo.