Jumatatu , 5th Nov , 2018

Nyota wa timu ya taifa Tanzania, Thomas Ulimwengu leo Novemba 5, 2018 amethibitisha kuachana na klabu yake ya Al Hilal ya nchini Sudan baada ya kutoridhishwa na baadhi ya vitu ndani ya klabu hiyo.

Thomas Ulimwengu mwenye jezi ya bluu.

 

 

Ulimwengu ambaye ameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu dhidi ya Lesotho, amesema mambo yanakwenda kinyume na alivyotarajia hivyo ameamua kuvunja mkataba.

''Akiongea kwa njia simu kutoka Sudan Ulimwengu ameweka wazi kuwa pande zote mbili zimefikia makubaliano ya kuvunja mkataba kwa makubaliano maalum hivyo hakuna tatizo kwani wamekubaliana vizuri'', amesema.

Hatua ya Ulimwengu kuvunja mkataba na Al-Hilal ikiwa si zaidi ya miezi mitatu tu tangu ajiunge nayo akitokea AFC Eskilstuna ya Sweden.

Ulimwengu hajaweka wazi ni timu gani ataelekea ila kwasasa atatua kwenye kambi ya Taifa Stars kujiandaa na mchezo huo.