Jumatano , 13th Sep , 2023

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania TFF Bwana Wallace Karia amesema matarajio yake ni kuona timu za Simba SC ,Yanga SC na Singinda Fountain Gate FC zinatinga hatua ya makundi ya mashindano ya kimataifa ambazo yanashiriki kwa hivi sasa.

Rais wa TFF Wallace Karia

Akizungumza na Waandishi wa Habari Rais Karia amesema kuwa anawatakia kila la kheri katika mechi zao  hizi na pia anaaamini watapata ushindi katika mechi zao zinazochezwa wiki hii huku akiwataka watanzania kuwa kitu kimoja katika kusapoti timu zetu hizi.

“Singida Fountain Gate Fc wanaanzia Nyumbani hivyo wamalize shuhuli hapa nyumbani na Simba SC na Yanga SC wanacheza ugenini mimi na uhakika watafanya vizuri katika mechi zao na pia napongeza ushirikiano mzuri ambayo umefanya na Maafisa habari wa vilabu hivyo kuungana na kushirikiana katika michuano hii ya Kimataifa”amesema Rais Karia .

Kwa upande mwingine Rais Karia ameleezea dhamira yao kwasasa wanakwenda kwenye  Mashindano ya Afcon nchini Ivory Coast si kwenda makundi tu bali  kwenda mbele zaidi.

Hii inakuwa mara ya tatu kwa Taifa Stars kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ambapo kwa mara ya kwanza ilifanya hivyo mwaka 1980 katika Fainali zilizochezwa nchini Nigeria, kisha mwaka 2019 nchini Misri na sasa inakwenda Ivory Coast.