Jumatatu , 5th Nov , 2018

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kamati yake ya Maadili, leo Novemba 5, 2018, limetangaza kumfungia maisha kutojihusisha na soka aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati yake ya Uchaguzi, Wakili Revocatus Kuuli.

Wakili Revocatus Kuuli

Taarifa za awali zinaeleza kuwa Wakili huyo msomi amekutwa na hatia ya kuweka hadharani nyaraka za shirikisho hilo na kuzisambaza kwa watu wasiohusika. 

Awali kikao cha kama ya Utendaji ya TFF kilimfikisha Kuuli mbele ya kamati ya maadili ambapo kamati hiyo imekuja na uamzi huo wa kumfungia maisha.

Kuuli ndiye alisimamia uchaguzi mkuu wa TFF Agosti 12, 2017, uchaguzi ambao ulifanyika jijini Dodoma na kumweka madarakani Rais wa sasa wa TFF Wallace Karia.