
Nembo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Ratiba hiyo imetolewa baada ya kikosi kazi kilichopewa kazi maalumu ya kupitia upya ratiba ya mashindano hayo na kukamilisha majukumu yake na kuweza kuruhusu kuendelea mwisho wa juma hili.
Kwa mujibu wa ratiba mpya, Septemba 9 mwaka huu (2017), timu ya Tanzania Prison FC itakutana na Majimaji FC katika uwanja wa Sokoine uliyoopo mjini Mbeya saa 10:00 jioni huku Azam FC akichuana na Simba SC katika dimba lao la nyumbani 'Azam Complex majira ya saa 1:00 usiku.
Unaweza kusoma ratiba kamili ya michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara hapa chini.