Jumanne , 11th Mar , 2014

Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limeridhia uamuzi wa kulipa fedha kutokana na kuharibiwa viti uwanja wa taifa.

Shirikishola soka nchini Tanzania TFF limesema linakubaliana na hatua iliyochukuliwa na serikali ya kulitaka shirikisho hilo kuhakikisha linalipa gharama zote zilizotokana na uharibifu wa viti uliofanywa na watu wasiojulikana katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam wakati wa mechi ya Yanga dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Afisa Habari wa TFF Bonifasi Wambura amesema hatua hiyo ya serikali ni sahihi na wao kama TFF watahakikisha gharama hizo zinalipwa.

Hata hivyo Wambura amesema TFF inakaa kuangalia ni hatua gani zinastahili kuchukuliwa kwa wahusika wa tukio hilo, na watahakikisha wanatengeza kanuni ambazo zitasaidia klabu au mashabiki watakaobainika kufanya vitendo hivyo kuchukuliwa hatua kali za kisheria.