Ijumaa , 23rd Nov , 2018

Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limeitaka klabu ya Yanga kubadilisha jina la klabu hiyo toka kuwa Sports Club (SC) na kuwa Football Club (FC), ambalo litaitambulisha kama Yanga FC.

Nembo ya klabu ya Yanga

Kupitia taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo, Yanga inatakiwa kufanya mabadiliko hayo haraka iwezekanavyo imesema kwa mujibu wa mwongozo kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

FIFA inavitaka vilabu vya soka kujihusisha na shughuli za mchezo wa soka pekee tofauti na michezo mingine, ambapo uwepo wa neno SC katika jina la klabu ni kumaanisha kuwa klabu hizo zinajishughulisha na michezo mingine tofauti na soka.

Soma zaidi katika taarifa rasmi ya TFF hapa chini.