
Baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa kufunga kozi ya mafunzo ya soka kwa wanawake, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Celestine amesema, kozi hizo zitalenga kuelimisha jamii kuhusu soka la wanawake pamoja na kulitangaza nchi nzima hususani vijijini.
Mwesigwa amesema kozi zitakazofuata zitahusisha masuala ya lishe pamoja na tiba kwa upande wa soka la wanawake ili kuhakikisha wanakuwa na madaktari pamoja na watu watakaohusika na lishe kwa wachezaji hapa nchini.
Celestine Mwesigwa (Kulia) - Katibu Mkuu TFF
Mwesigwa amesema, pia ubalozi wa nchini Sweden umeahidi kushirikiana na TFF ili kuhakikisha rasilimali zinapelekwa katika soka la wanawake ili kulikuza na kulisambaza zaidi hapa nchini.