Jumanne , 6th Feb , 2024

Timu ya Tenesi ya Tanzania kwa Watu wenye Ulemavu (WeelCheer Tennes) itashiriki katika mashindano ya Afrika yanayofanyika nchini Nigeria yenye lengo la Kufuzu katika machindano ya Dunia,pamoja na mashindano ya paralimpic.

Nchi Kumi na sita 16 za Afrika zitashiriki katika mashindano hayo,na Kikosi cha Tanzania kinajumla ya wachezaji sita 6,wakiume watatu 3 na wakike watatu 3

Kocha wa Timu ya Tennes ya Tanzania kwa Watu wenye Ulemavu riziki Salum ,amesema wachezaji wote wameanza maandalizi mapema hivyo watanzania watarajia mambo mazuri.

''Ni mashindano ambayo wachezaji yatawaongezea nafasi za kupanda na kushuka iwapo wakifanya vizuri''amesema kocha.