Ijumaa , 12th Jul , 2024

Timu ya Tanzania ya Kriketi chini ya umri wa miaka 19 inazidi kujifua vikali kujiandaa na shindano la kuwania kufuzu Kombe la Dunia kwa kanda ya Afrika ambalo linataraji kufanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 31-2024.

Timu ya Tanzania ya Kriketi chini ya umri wa miaka 19

Akizungumzia maandalizi kuelekea kwenye shindano hilo,Kocha Msaidizi wa timu ya Tanzania Salum Jumbe amesema ameona mabadiliko makubwa baada ya kupata michezo miwili ya kirafiki huku ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye shindano hilo.

''Kikosi kinaendelea na kambi na wachezaji wote wana morali ya kuhakikisha wanapata nafasi ya kuiwakilisha nchini katika michuano hiyo''amesema Kocha Salum Jumbe

Kwa upande mwingine,Wachezaji wa timu hiyo wameshukuru mafunzo wanayoyapata kutoka kwa walimu wao huku wameahidi kufanya vyema na kukata tiketi ya kushiriki kwenye kombe la Dunia kwa mchezo wa Kriketi chini Umri wa miaka 19.

Shindano hilo linataraji kushirikisha nchi za Sierra Leone,Botswana,Rwanda,Msumbiji,Malawi,Nigeria na Ghana huku shindano hilo linataraji kuanza Julai 31 mpaka Agosti 12-2024