Ijumaa , 10th Jul , 2015

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 20 (Tanzanite) kesho itashuka dimbani uwanja wa Azam Complex kucheza na timu ya Taifa ya Zambia chini ya miaka 20 (Young She-Polopolo).

Mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Wanawake za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Papua New Guinea, utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Sudan ambao tayari wameshawasili hukuYoung She-Polopolo ikiwa nayo imeshwasili nchini jana jioni, na leo wakiwa wamefanya mazoezi mepesi kwa ajili ya mchezo huo.

Kizuguto amesema, Tanzaniate imejiandaa vya kutosha ikiwa chini ya Kocha Rogasian Kaijage huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kuchezwa baada ya wiki mbili ambapo itakuwa ni Julai 25 Lusaka, Zambia.