Jumapili , 6th Apr , 2014

Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imetinga fainali za mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto wa Mitaani baada ya kuichapa Marekani mabao 6-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliochezwa jana (Aprili 5 mwaka huu) jijini Rio de Janei

Baadhi ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kwa watoto wa mitaani.

Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imetinga fainali za mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto wa Mitaani baada ya kuichapa Marekani mabao 6-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliochezwa jana (Aprili 5 mwaka huu) jijini Rio de Janeiro, Brazil.

Hadi mapumziko Tanzania ilikuwa mbele kwa mabao 4-0. Bao pekee la Marekani katika mchezo huo ambayo hadi nusu fainali ilikuwa haijafungwa lilifungwa dakika za mwisho.

Kwa matokeo hayo, Tanzania inacheza nusu fainali na Burundi. Mechi hiyo inachezwa leo (Aprili 6 mwaka huu) ambapo Burundi imetinga hatua hiyo baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika nusu fainali ya pili.

Mchezo huo wa fainali unachezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense katikati ya Jiji la Rio de Janeiro huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza, George Osborne.

Katika mechi ya kwanza katika kundi B la michuano hiyo, Tanzania ilicheza na Burundi na kutoka sare ya mabao 2-2.