Jumamosi , 29th Mei , 2021

Kocha msaidizi wa klabu ya soka ya Simba, Selemani Matola amethibitisha taarifa kuwa mchezaji Clatous Chama amefiwa na mke wake, Mercy Chama.

Clatous Chama akiwa na mke wake Mercy

Amesema hayo muda mchache kabla ya kuanza kwa mechi ya Namungo FC dhidi ya Simba katika Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi.

Amesema wamepokea taarifa za kifo hicho mchana wa leo, ikiwa ni baada ya kuugua kwa muda akiwa nchini kwao Zambia.

"Tumepata taarifa hizi mchana wa leo na baada ya mchezo dhidi ya Namungo klabu itapanga namna ya kushughulikia suala hili", amesema Matola.