Ijumaa , 9th Jan , 2015

Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kinatarajia kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda itakayofanyika Januari 22 mwaka huu uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Sika nchini TFF, Boniface Wambura amesema mechi hiyo ni sehemu ya programu ya Kocha Mart Nooij kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya mechi za mchujo michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN).

Wambura, amesema Mechi za mchujo za michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Rwanda zinaanza Mei mwaka huu.

Wambura amesema, Kocha Nooij anatarajia wakati wowote kutangaza kikosi cha timu hiyo ambacho kinatarajiwa kuingia kambini Januari 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam, ambayo ni siku moja baada ya kwenda jijini Mwanza.