
Kikosi cha Stars kikiendelea na mazoezi kwa ajili ya kuvaana na Algeria Novemba 14
Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF Mwesigwa Celestine amesema, kikosi hicho kinaendelea na mazoezi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kujenga uelewano katika mchezo baina ya wachezaji waliopo katika kikosi hicho.
Mwesingwa amesema, kikosi cha timu ya taifa ya Algeria kinatarajiwa kuwasili nchini siku ya Ijumaa ya Novemba 13 huku msafara wa awali ambao ni watangulizi wanaokuja kwa ajili ya kuandaa mazingira ya malazi kwa timu ya Algeria wanatarajiwa kuanza kuwasili leo hii usiku.
Mchezo wa hatua ya pili kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia zitakazofanyika mwaka 2018 nchini urusi kati ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Algeria (The Fox Desert) utafanyika tarehe 14 Novemba, 2015 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
kikosi cha Stars chini ya kocha mkuu Charles Mkwasa kimefanikiwa kusonga hatua ya pili ya michuano hiyo baada ya kuiondosha Malawi (The Flames) kwa jumla ya mabao 2-1, nyumbani ikishinda 2-0, na kufungwa 1 – 0 jijini Blantyre.