Jumatatu , 6th Apr , 2015

Mechi kati ya Stand United na Mtibwa Sugar iliyoahirishwa hapo jana imemalizika hii leo kwa timu ya Stand United kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Uwanja wa Kambarage Mjini Shinyanga.

Bao hilo lilifungwa jana na kiungo Haroun Chanongo ambapo baada ya goli hilo mechi hiyo iliahirishwa katika dakika ya 33 kutokana na Uwanja kujaa maji yaliyotokana na kunyesha Mvua Kubwa.

Kwa upande wa Simba SC wanatarajia kukaribishwa na Kagera Sugar uwanja wa Kambarage mjini humo baada ya mechi hiyo miliyotakiwa kuchezwa siku ya Jumamosi kuahirishwa pia kutokana na Mvua kubwa kunyesha na kupelekea uwanja kujaa Maji.