Dan Sserunkuma
Mchezaji wa Simba Daniel Sserunkuma amesema lengo lake hasa kuwa katika timu hiyo sio kuipatia magoli pekee bali ni kuisaidia timu hiyo kufikia malengo waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kunyakua Ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara na kushiriki mashindano mbalimbali makubwa.
Akizungumza na East Africa Radio, Sserunkuma amesema hana uzoefu mkubwa katika ligi ya Tanzania lakini anatarajia kucheza mechi nyingi zaidi ili kuweza kupata uzoefu katika ligi hii yenye ushindani.
Sserunkuma amesema anatarajia ligi itakuwa ngumu na yenye ushindani lakini kutokana na kujiamini na mazoezi anayoendelea kufanya,anaamini atafanya vizuri ili kutimiza yale yote aliyoyaahidi.
Kwa upande wake Mchezaji Hassan kessy aliyesajiliwa na Klabu hiyo akitokea timu ya Mtibwa Sugara amesema ushindani ni mkubwa katika timu hiyo na sio rahisi kuweza kupata namba ila kama mchezaji akionesha juhudi katika mazoezi na nidhamu ya kimchezo ataweza kufanya vizuri katika kikosi hicho.
Kessy amesema wapinzani wao ambao ni Yanga ni wazuri na unapokuwa unacheza nao unatakiwa kuwa makini kutokana na kila timu kutokubali kushindwa hivyo anahakikisha atafanya vizuri katika kikosi hicho kama alivyokuwa akifanya alipokuwa akiichezea Mtibwa Sugar.