Jumapili , 18th Aug , 2019

Kampuni ya vinywaji ya Coca-Cola, imesema itaendeleza vipaji vya vijana kupitia sekta michezo kwa kuandaa mashindano yatakayowakunatisha vijana, kwa nia ya kukuza vipaji vyao pamoja na kuwatengenezea fursa za ajira.

Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Umma na Mawasiliano wa Coca-cola ambayo inazalisha kinywaji cha Sprite, Haji Mzee Ally wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Sprite Bball Kings msimu wa 2019.

Mzee amesema kuwa "ahadi yetu kama Coca-Cola ni kuendelea kuwa mstari wa mbele hasa linapokuja suala la kuwasaidia vijana, katika kuendeleza vipaji vyao ambavyo vitaleta mabadiliko katika maisha yao"

"Tumelidhihirisha zaidi kupitia majukwaa mengine ya kuibua vipaji kama vile Coke Studio Afrika, East Africa Got Talent na mashindano ya COPA Coca-Cola." amesema Haji Mzee Ally

Jana Agosti 17, 2019 msimu mpya wa mashindano ya Sprite Bball Kings kwa mwaka 2019 ulifunguliwa ambapo zaidi ya timu 30 zilijitokeza kujiandikisha kwa kushiriki michuano hiyo.