Jumapili , 30th Mei , 2021

Msafara wa watu 27 kutoka Senegal uliowakilisha nchi katika mashindano ya soka la ufukweni kwa ukanda wa Africa 'BSAFCON2021' umeanza safari kurejea nchini kwa kutumia shirika la ndege la Ethiopian Airline na wanatarajia kufika nchini usiku wa kuamkia jumatatu

Wachezaji wa timu ya soka la ufukweni wakiwa uwanja wa ndege Senegal

Katika mashindano hayo, timu ya taifa ya Senegal ambao ndiyo wenyeji wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa huo wa BSAFCON2021 baada ya kuwafunga Msumbiji magoli 4-1 katika mchezo wa fainali iliyofanyika jumamosi tarehe 29/05/202.

Mashindano hayo yaliyoshirikisha mataifa 7 toka Africa yamemalizika kwa Senegal wenyeji kutwaa ubingwa , nafasi ya 2 Msumbiji 3 Morocco 4 Uganda 5 Misri 6 Tanzania 7 Shelisheli

Mashindano hayo yamewapa Senegal na Msumbiji tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia mwaka baadaye mwaka huujkatika jiji la Moscow nchini Urusi kwa kushirikisha mataifa zaidi ya 16 kutoka mabara 6

Tanzania tunarejea tukiwa mikono mitupu baada ya kupoteza michezo yote mitatu tuliyocheza miwili kwenye kundi na moja dhidi ya Misri kugombea nafasi ya tano.