Jumapili , 14th Jul , 2024

Kikosi cha Yanga kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Augusburg inayocheza Ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani, mchezo huo utakuwa katika ligi ya muda mfupi ya Mpumalanga Primier International Cup itakayofanyika kuanzia Julai 20-27 nchini Afrika Kusini.

Ligi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya, timu nyingine zinazotarajiwa kushiriki ni Mbabane Swallows na TS Galaxy.

Hata hivyo bado Yanga hawajatoa taarifa rasmi za kuthibitisha kushiriki wao katika michuano hiyo lakini wamethibitisha kucheza michuano ya Kombe la Toyota ambapo Julai 28 watacheza dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.