Bingwa mtetezi wa Wimbledon upande wa Wanawake, Simona Halep akishangilia moja ya taji lake alilotwaa katika michuano.
Raia huyo wa Romania alitonesha jeraha lake katika michuano ya wazi ya Italia hali iliyopelekea pia kutoshiriki michuano ya wazi ya Ufaransa iliyopita.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29, alionekana katika viunga vya London nchini Uingereza akionekana kuwa alikuwa tayari kutetea ubingwa ambao aliutwaa mwaka 2019.
Halep anaungana na mchezaji namba mbili katika viwango vya ubora Duniani upande wa wanawake, Naomi Osaka ambaye na yeye amejiondoa kutokana na matatizo ya kiafya.

