Jumatatu , 8th Apr , 2024

Mwanariadha kutoka Tanzania Alphonce Felix Simbu amenyakua medali ya shaba baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu katika mbio za Daegu Marathon nchini Korea Kusini.

Simbu ni mwanariadha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ametumia masaa 2:07:55 kumaliza mbio hizo nyuma ya Stephen Kiprop; 2:07:04 na Kennedy mutai; 2:07:40 kutoka Kenya.