Jumanne , 6th Nov , 2018

Klabu ya soka ya Simba imeweka wazi wachezaji wake ambao itawatumia kwenye michuano ya kimataifa hususani ligi ya mabingwa Afrika msimu wa 2018/19.

Wachezaji wa Simba

Jumla ya wachezaji 25 wamejumuishwa katika orodha hiyo na majina yao kutumwa makao makuu ya shirikisho la soka barani Afrika (CAF).

Simba imetuma majina ya makipa wawili ambao ni Aishi Manula na Deogratius Munishi.

Mabeki ni Shomari kapombe, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Paul Bukaba, Yusuph Mlipili, Salimin Mbonde, Juuko Murshid na Asante kwasi.

Viungo ni Jonas Mkude, James Kotei, Mzamiru Yassin, Said Ndemla, Hassan Dilunga, Shiza Kichuya, Haruna Niyonzima, Clatous Chota Chama, Mohammed Ibrahim na Rashid Juma.

Washambuliaji ni John Bocco, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na Adam Salamba. CAF inatarajia kupanga mechi za raundi ya awali za michuano hiyo mapema tu baada ya mechi fainali ya ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho msimu wa 2017/18.