
Shomari Kapombe
Kapombe amesaini mkatab wa miaka miwili mbele ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba Mohammed Dewji, leo Juni 27, 2019.
''Beki bora wa kulia nchini Shomari Kapombe amesaini mkataba mpya wa miaka miwili ambao utamwezesha kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Mabingwa'', wameeleza Simba.
Aidha Simba imetumia nafasi hiyo kueleza hali ya kiafya ya Kapombe ambaye alikuwa anasumbuliwa na goti tangu Novemba 2018, alipoumia kwenye kambi na timu ya taifa ya Tanzania.
''Shomari kwa sasa yupo fiti kucheza na atakuwa sehemu kikosi ambacho kitaenda nje ya nchi kujiandaa na msimu mpya'', wameongeza.