Jumanne , 27th Jan , 2015

Klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam imeliomba Shirikisho la Soka nchini TFF kuchunguza matukio yaliyojitokeza katika mechi waliyocheza dhidi ya Azam.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Stephen Ally amesema katika mechi hiyo kulikuwa na matukio mbalimbali moja likiwa la mchezaji wa Klabu hiyo Emmanuel Okwi ambaye alifanyiwa madhambi na Beki wa Azam Agrey Morris iliyopelekea Okwi kupoteza fahamu.

Ally amesema, vyombo vinavyohusika wanatakiwa kufuatilia ripoti ya msimamizi wa mashindano pamoja na mwamuzi ili kuweza kuchukua hatua kwa mchezaji aliyefanya makosa katika nmechi hiyo kuchukuliwa hatua.

Ally amesema, katika mechi hiyo kulikuwa na makosa mbalimbali yaliyochangia wachezaji kuweza kupoteza umakini suala lililochangia pia kushuka kwa kiwango cha wachezaji katika mchezo huo.

Kwa upande mwingine, Ally amesema timu ya Simba chini ya Miaka 20 imeanza mazoezi rasmi ambapo itaanza kuingia katika mechi za utangulizi hapo kesho ambapo hapo awali ilikuwa ikishindwa kuingia kutokana na matatizo ya kimfumo ambayo wameshayafanyia kazi.