Alhamisi , 9th Mar , 2017

Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt. Ashatu Kijaji amezitaka kampuni zinazotoa huduma ya mawasiliano nchini kuharakisha mchakato wa kujisajili katika soko la awali la hisa

Kikosi cha Simba

Mechi mbili za kwanza hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho sasa zitachezwa Machi 18 na 19, mwaka huu kwenye viwanja viwili tofauti.

Mechi hizo ni kati ya Kagera Sugar itakayocheza na Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani Kagera wakati siku inayofuata Machi 19 Simba itacheza na Madini kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Awali Simba ilikuwa icheze Machi 18, mwaka huu, lakini taarifa iliyotolewa na TFF leo imesema kuwa siku hiyo uwanja huo utakuwa na shughuli za kijamii hivyo sasa utachezwa siku ya Jumapili Machi 19, mwaka huu.

Taarifa hiyo imesema kuwa mechi nyingine zitapangiwa tarehe za baadaye.

Yanga walipoichapa Kiluvya United bao 6-1 na kutinga robo fainali

Mechi hizo ni kati ya Azam FC na Ndanda FC kadhalika Tanzania Prisons ya Mbeya itakayocheza na Young Africans ya Dar es Salaam.

Bingwa wa michuano hiyo kwa mujibu wa kanuni, atazawadiwa Tsh. 50 milioni.

Pia bingwa wa michuano hiyo, ndiye atakayeiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika wakati Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ndiye ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Total Ligi ya Mabingwa Afrika.