Jumamosi , 12th Sep , 2015

Pazia la Ligi kuu Tanzania Bara limefunguliwa leo huku ikishudia timu saba zikishuka dimbani na vipigo vikitawala katika baadhi ya viwanja.

Kikosi cha Simba kilichoshuka dimbani leo kukabiliana na African Sports

Pazia la Ligi kuu Tanzania Bara limefunguliwa leo huku ikishudia timu saba zikishuka dimbani na vipigo vikitawala katika baadhi ya viwanja.

Washindi wa pili katika msimu uliopita timu ya Azam FC imeanza mchezo wake ikiwa nyumbani katika viwanja vya Chamanzi ambapo imeweza kuutimia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wajelajea wa Prison kutoka jijini Mbeya.

African Sports wana kimanumanu ya jijini Tanga imeshindwa kufanya vizuri katika uwanja wake wa nyumbani baada ya kuchapwa bao moja kwa bila na timu ya Simba Sports Club.

Bao la mchezo huo liliwainua mashabiki wa Simba waliokuwa wakishangilia katika viwanja vya Mkwakwani jijini humo ikiwa bao hilo lilifungwa mnamo dakika ya 56 na mchezaji Hamis kiiza baada ya kupokea kona nzuri kutoka kwa Musa Hassan Mgosi.

Timu ya soka ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara imeshindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani wa Nangwanda Sijaona, baada ya kulazimishwa sare ya goli 1-1 na Mgambo JKT ya Tanga, katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara.

Ndanda ndio walioanza kupata goli kupitia kwa mshambuliaji wao mpya Atupele Green, aliyefunga goli la mapema dakika ya pili ya mchezo baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Mgambo, kabla ya Fully Maganga kusawazisha katika dakika ya 72 kutokana na makosa binafsi yaliyofanywa na walinzi wa Ndanda.

Akizungumza baada ya mchezo huo, kocha wa Ndanda SC, Amimu Mawazo, amekiri kuwepo kwa makosa yaliyofanywa na wachezaji wake kiasi cha kuwakosesha kuondoka na pointi tatu katika mchezo huo.

Matokeo Mengine
Majimaji 1-0 Ruvu JKT
Toto Afrika 1-0 Mwadui
Kagera Sugar 1- 0 Mbeya city
Mtibwa 1-0 Stand United

Ligi hiyo inaendelea tena Kesho ambapo mabingwa timu ya Yanga watashuka Dimbani dhidi ya Timu ya Coastal Union ya Jijini Tanga ambapo msimu uliopita walichapwa magoli 8-0.