Jumatatu , 21st Nov , 2016

Uongozi wa klabu ya Simba umeitisha mkutano wa wanachama wa dharura utakaofanyika Desemba 11 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Mashabiki wa Simba uwanjani

 

Msemaji wa Simba Haji Manara amesema, mkutano huo umeitishwa baada ya kikao cha kamati  ya utendaji wa klabu hiyo iliyokaa Novemba 18 mwaka huu.

“Kamati ya utendaji imetoa baraka zake kupitia ibara ya 22 ya katiba ya Simba na mkutano huo utakuwa ni muendelezo wa mkutano wa kawaida uliofanyika Julai 31 mwaka huu” amesema Manara.