Jumatano , 11th Sep , 2024

Uongozi wa klabu ya Simba SC umesema kuwa katika mchezo wa kwanza wa kombe la shirikisho la barani Afrika dhidi Al Ahly Tripoli,Libya utaopigwa jumapili hii ya septmba 15 , 2024 utakuwa ni mchezo mgumu lakini wamejipanga kupata matokeo mazuri kwaajili ya kutimiza malengo

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja habari na mawasiliano wa Simba Ahmedy Ally amesema kuwa wanakwenda kukutana na mpinzani ambae ana historia nzuri hivyo licha ya kuwa ndiyo kwanza wanatengeneza timu yao.  

''Tunakwenda na kikosi chetu naamini utakuwa ni mchezo mzuri na ushindi tunawategemea kwa wachezaji wajitume kwaajili ya kupata ushindi''amesema Ahmedy Ally.

.kikosi cha Simba SC kimeondoka leo asubhi  kwenda Tripoli nchini Libya  kwaajili ya mchezo  wa kwanza hatua  ya  32 bora  wa kombe la shirikisho barani Afrika  na mshindi wa jumla wa mchezo huo atafuzu hatua ya 16 bora  ambayo itachezwa kwa mtindo  wa makundi .