
Zacharia Hans Poppe ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, pamoja na wajumbe Said Tully na Collins Frisch, jana walikuwa uwanjani wakati Zambia ikiitwanga Malawi kwa mabao 3-0, jana. Lengo ni kumalizana na kocha wa timu ya taifa ya Zimbabwe.
Viongozi hao walikuwa wakimsubiri kocha wa Kalisto Pasuwa amalize mechi ili wafanye naye mazungumzo na mara baada ya mechi kuisha wakiongozwa na Hans Poppe walifanikiwa kufanya mazungumzo na kocha huyo na amekubali kutua Simba.
Mpaka sasa ni mambo machache yamebaki na anahitaji kupata maslahi yake anayodai Zimbabwe, hivyo juhudi bado zinafanyika kwasababu na yeye ameshaona mazingira ya mkataba wa Simba na amekubaliana nao.
Pasuwa ndiyo chaguo la kwanza la Simba, ikishindikana kabisa, Simba imepanga kumuajiri kocha raia wa Senegal na Joseph Omog kocha wa zamani wa Azam FC raia wa Cameroon, yeye anaonekana kuwa chaguo la tatu.