Jumatano , 19th Nov , 2014

Klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam imesema inaendelea na mazungumzo na Mabingwa watetezi wa Kombe la Ligi kuu Tanzania Bara,Azam Fc kuhusu kumsajili mchezaji wao Amri Kiemba.

Mchezji wa Simba Sc,Amri Kiemba

Akizungumza na East Africa Radio,Afisa habari wa Klabu hiyo,Humphrey Nyasio amesema uongozi wa timu hizo mbili zinaendelea na mazungumzo ambapo hapo awali timu ya Azam iliomba kumchukua mchezaji huyo kwa mkopo suala ambalo walishindwa kufikia makubaliano.

Nyasio amesema mpaka sasa hawajapokea barua yoyote kutoka kwa Kiemba kuhusu kuvunja mkataba na klabu hiyo kama inavyoripotiwa na watu mbalimbali hapa nchini.