Jumatano , 31st Dec , 2014

Michuano ya Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuanza kutimua vumbi hapo kesho Uwanja wa Amaan Zanzibar huku wenyeji wa michuano hiyo JKU akifungua na Mafunzo katika kundi A ikifuatiwa na mechi ya Simba dhidi ya Mtibwa.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu wa kamati ya michuano hiyo, Khamis Said amesema timu shiriki zipo 12 ambapo ni sita kutoka nje ya Zanzibar na sita kutoka Zanzibar ambapo zimegawanywa katika makundi matatu huku kila timu ikiwa na makundi manne.

Said amezitaja timu hizo kuwa ni Yanga, Simba, Azam na Mtibwa Sugar zote kutoka Tanzania Bara huku KCC na Sport Villa zikitokea nchini Uganda.

Saidi amesema timu za Zanzibar zitakazoshiriki michuano hiyo ni KMKM, Mtendeni Ranger, Shaba, Polisi, JKU na Mafunzo.

Said amesema, fainali za michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa Januari 13 usiku katika Uwanja wa Amaan kwa kuhitimisha michuanoi hiyo.

Ratiba nzima ya michuano hiyo ni hii hapa;-

Alhamis 1 Januari 2015
Jioni Saa 9:00 JKU vs MAFUNZO............ KUNDI C
Jioni Saa.11:00. POLISI VS SHABA............KUNDI . A
Usiku Saa 2:15. SIMBA VS MTIBWA.........KUNDI C

Ijumaa 2 Jan 2015
Jioni saa 10:00 KMKM VS MTENDE ….........KUNDI B
Usiku Saa 2:00 KCC VS AZAM........KUNDI B

Jumamosi 3Jan 2015.
Jioni Saa 10:00 JKU VS MTIBWA..........KUNDI C
Usiku Saa 2:00 YANGA VS SC.VILLA..........KUNDI A

Jumapili 4 Jan 2015
Jioni saa 9:00 KCC VS MTENDE............KUNDI B
Jioni saa 11:00 KMK VS AZAM..............KUNDI B
Usiku saa 2:15. MAFUNZO VS SIMBA............KUNDI C

Jumatatu 5 Jan 2015
Jioni saa 10;00 SC VILLA VS SHABA.............KUNDI A
Usiku saa 2:00 YANGA VS POLISI...............KUNDI A

Jumanne 6 Jan 2015
Jioni saa 9:00 AZAM VS MTENDE....... KUNDI B
Jioni saa 11: 00 MTIBWA VS MAFUNZO.....KUNDI C
Usiku saa 2:15. SIMBA VS JKU........KUNDI C

Jumatano 7 Jan 2015
Jioni saa 9;00 POLISI VS SC VILLA ....KUNDI........ A
Jioni saa 11:00 KCC VS KMKM............KUNDI B
Usiku saa 2:15. YANGA VS SHABA...........KUNDI A

Alhamisin 8 Jan 2015.
Jioni saa 10:00WINNER.........B VS RUNNERS..............A.
Usiku saa 2:00 WINNER...........A VS BEST LOOSER.......1

Ijumaa 9 Jan 2015
Jioni saa 11:00 WINNER C VS BEST LOOSER 2
Usiku saa 2;00 RUNNERS. VS RUNNERS..............C.

Jumapili 11 Jan 2015.
SEMIFINAL 1
Jioni saa 10:00.WINNER 1 VS WINNER 2
SEMIFANAL 2
Usiku saa 2:00WINNER 3 VS WINNER 4