Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Dokta Sulemani Serera katika hafla ya kuaga na kukabidhi bendera timu ya Tanzania itakayoshiriki michezo ya Olimpiki itakayoanza Julai 26 mpaka Agosti 11 mjini Paris nchini Ufaransa.
"Mwaka huu tunawakilishwa na wachezaji saba lengo letu ni kuona mwaka 2028 tunapeleka idadi kubwa ya wachezaji na Serikali itaendelea kushirikiana na Mashirikisho ya Michezo ili kufikia malengo yetu, amesema Serera.
Upande mwingine,Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi amesema maandalizi ya msafara wa Tanzania yamekamilika huku msafara huo utakuwa na awamu tatu kwenda kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki ya Paris 2024
“Timu hiyo itaondoka kwa makundi ambapo kundi la kwanza litaondoka litaondoka Julai 22 (mkuu wa msafara) kundi la pili Julai 23 (kuogelea) na kundi la mwisho litaondoka Julai 27( riadha)” amesema Filbert Bayi
Tanzania katika Michezo ya Olimpiki Paris 2024 itawakilishwa na Wanamichezo 7 ambao ni Wanariadha 4,Waogeleaji 2 na mchezaji wa Judo 1.